Jumla ya kiasi cha Tshs.48,259,947,369.00 zimeidhinishwa na kupitishwa na baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Same ikiwa ni makisio ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021. Kati ya fedha hizo Tshs. 2,876,165,122.00 Ruzuku ya miradi ya maendeleo, Tshs.2,073,922,630.00 ruzuku ya matumizi ya Kawaida, Tshs. 41,087,648,617.00 mishahara na Tshs. 2,222,211,000.00 mapato ya ndani.
Akiwasilisha makisio na mpango wa bajeti, kwa niaba ya Mkurugenzi, Simeon V Mzee ambaye ni Afisa Mipango wa Halmashauri alisema kuwa,makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 yameongezeka kutoka Tshs 36,294,106,325.00 mwaka 2019/2020 hadi Tshs 48,259,947,369.00 ikiwa ni ongezeko katika bajeti ya mishahara.Matumizi mengineyo(Ruzuku) yatagharimu Tshs 2,073,922,630.00 ambapo vipaumbele katika fedha hizi ni pamoja na shughuli za uendeshaji utawala na usimamizi,gharama za likizo,uhamisho,matibabu na maslahi mengine ya watumishi,uendeshaji wa vikao vya kisheria na stahiki za waheshimiwa madiwani,mitihani kwa shule za msingi na sekondari,gharama za kuitwa kazini kwa watumishi wa afya na ununuzi wa dawa.
Mapato ya ndani bajeti ni Tshs 2,222,211,000.00 imezingatia maeneo makuu mawili ambapo ni kuchangia miradi ya maendeleo Tshs 593,444,652.00 sawa na 40% ya makusanyo halisi na matumizi ya kawaida Tshs 890,166,978.00 sawa na 60% ya makusanyo halisi ambapo matumizi kupitia ICHF ni Tshs 119,836,142.00,matumizi kupitia NHIF ni Tshs 258,608,228.00,malipo ya papo kwa papo(user fee) ni Tshs 133,117,000.00,ada za shule za kidato cha tano na sita ni Tshs 67,200,000.00 na michango ya wadau kwenye elimu ni Tshs 159,838,0
Ndugu Simeon Mzee alivitaja vipaumbele kuwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri,kukuza sekta ya viwanda ndani ya Halmashauri,kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Same kwa kujenga hospitali mpya ya Wilaya,kuimarisha sekta ya utalii wa ndani kupitia vivutio vilivyopo,ukamilishaji wa miradi viporo iliyopo ndani ya Halmashauri na upatikanaji wa samani(viti,meza na madawati),upandaji miti na kuitunza ili kuboresha mazingira ya Wilaya,kuwezesha vijiji kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji na kuendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ili kuleta ustawi wa maisha na maendeleo yao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.