Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Edward J.Mpogolo anawa alika Wananchi wote wa Wilaya ya Same,wageni na wakazi wa maeneo jirani kushiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru utakaopokelewa katika kata ya Bendera ukitokea Mkoani Tanga Wilaya ya Korogwe Tar 6/6/2022.
Mwenge utatembelea,kuzindua na kuweka jiwe la Msingi katika Miradi mbalimbali inayo tekelezwa na Serekali ya Awamu ya Sita kisha kutakuwa na sherehe na shamrashamra za Mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Stendi kuu ya Mabasi Same Mjini ambapo vitakuwepo vikundi mbalimbali vya wasanii,Ngoma za asili ya kipare ikiwa ni pamoja na Kajanja,Muziki na Sinema wakati wote wa Mkesha.
Usipitwe na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Same.
Kauli Mbiu "SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO;SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA"
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.