• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

WILAYA ZOTE FANYENI MATAMASHA YA UTALII-DKT CHANA

Posted on: December 22nd, 2024

Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Balozi.Dkt. Pindi Chana ( Mb) amezitaka Halmashauri zote  za wilaya nchini kuanzisha matamasha ya Utalii na Uhifadhi huku akielekeza suala la kuwalinda wananchi dhidi ya  wanyamapori wakali na waharibifu kuwa ajenda ya kudumu.

Mhe. Chana ametoa kauli hiyo  Desemba 21, 2024  wakati akimwakilisha Mhe. Waziri Mkuu kufungua rasmi msimu wa pili wa Tamasha la Utalii la Same ambapo pia ametoa zawadi  na tuzo kwa wadau mbalimbali kutambua mchango wao katika kufanikisha Tamasha hilo

"Wakati leo tunasherekea  Tamasha la pili la Utalii la Same ni lazima  tuhakikishe tunawalinda wananchi kutokana na wanyama wakali wakati huo huo tunahifadhi rasilimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu ili zitusaidie kutuletea watalii zaidi " amefafanua Mhe Chana.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TAMISEMI na  wananchi itaendelea kuhifadhi rasilimali kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha amefafanua kuwa usemi wa kiswahii usemao "Tunza mazingira yakutunze"  unadhihirisha kuwa mazingira yakitunzwa vizuri ikiwemo misitu na maliasili yatasaidia kujenga uchumi.

 "Tukitunza mazingira tutapata mvua, tutapata maji, tutalima, tutapata vyakula na mazao ya biashara, hakutakuwa na njaa wala umaskini wa kipato na pia tutaishi kutokana na Kuvuta hewa safi.Usemi huo una mashiko ni vyema tukarithisha watoto wetu kuanzia wawapo shuleni ili waweze kutambua umuhimu wa kutunza mazingira"ameongeza Mhe. chana

 Amesema ni muhimu klabu za mazingira zilizopo katika maeneo yetu kuendelea  kuzisimamia ili zilete tija kwani kupitia klabu hizo wanafunzi watajifunza hifadhi ya mazingira, utalii na pia watajenga uelewa wa kutosha kutenda popote wawapo kwa falsafa ya "Jenga kesho iliyo bora (BBT)".  

Amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuandaa Filamu ya Tanzania the Royal Tour na Amazing Tanzania ambapo amesema kuanzishwa kwa Tamasha la Utalii la Same ni  kufuata maono ya Mhe. Rais katika kutangaza utalii.

Akifafanua kuhusu faida ya Tamasha hilo amesema limesaidia kuwaletea wageni, pia kutoa elimu mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kama misitu wa Chome.

Pia kuhusu kuboresha na Tamasha hilo, Mhe. Chana ametaka kuwepo na mikakati madhubuti ya kuendeleza Tamasha hilo kwa  Halmashauri kutenga   bajeti kuliko kuwaachia wadau wachache na uongozi wa Wilaya hiyo huku akisisitiza kuwa suala la uhifadhi na utalii lipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.


"Ndugu zangu suala hili ni la msingi sana hata baba wa Taifa Mwalimu  Nyerere alisisitiza kuwa rasilimali hizi lazima zilindwe na ndiyo maana  tuna Jeshi la Uhifadhi"amefafanua Waziri Chana

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali kuwabaini watu waovu, wanaotaka kuhujumu  rasilimali za watanzania.

"Kuna changamoto za maingiliano  tuliangalie ili wasilete madhara".

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Metheusela Ntonda amesisitiza kuendelea kufungamanisha Utalii na utamaduni kwenye matamasha hayo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • DC KASILDA ATAKA WANANCHU KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI WAKATI WA ZIARA YA MWENGE WA UHURU

    June 10, 2025
  • WASHIRIKI UMISSETA WATAKIWA KUWAKILISHA VEMA WILAYA YA SAME

    June 09, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.