Wananchi wa Wilaya ya Same wametakiwa kuwa na vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka majumbani kwao na kwenye biashara zao ili kujilinda na magonjwa ya mlipuko.
Wito huo umetolewa na Afisa Afya wa Wilaya ya Same Bi.Yuster Malisa wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe Wilayani Same.
"Suala la kunawa mikono kwa maji tiririka ni muhimu kwa Afya ya kila mmoja wetu,hivyo ni vyema kila familia na wafanyabiashara kuweka kifaa cha kunawia mikono kwa maji tiririka "alisema Yuster.
Abasi Mshana ni mfanyabiashara wa chakula Wilayani Same ambaye anasema wananchi wengi kwasasa wanaelewa umuhimu wa kunawa mikono.
"Yangu ugonjwa wa Corona utusumbue wananchi wamekua Sana umuhimu wa kunawa mikono maana hata maji yakiisha ukichelewa kujazia wanakufuata kuhitaji maji"alisema.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.