• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

Posted on: June 18th, 2025

Wananchi  Wilayani Same wameonywa kutotumia njia zisizo rasmi kuunganishiwa huduma ya Maji kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na watakaobainika hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao.

Onyo hilo limetolewa Juni 16, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mheshimiwa Kasilda Mgeni, wakati wa kikao cha wadau wa maji kilichoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SAMWASA) wilayani humo.

 Mhe. Kasilda amesema vitendo vya wizi wa maji vimekuwa kikwazo kikubwa kwa Mamlaka hiyo kufikia malengo ya utoaji wa huduma bora ya maji kwa wananchi.

"Kuharibu miundombinu ya maji au kujiunganishia maji kwa njia ya wizi ni kosa kisheria na ukikutwa utashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi"alisema Mhe. Kasilda

Aidha, amewataka wananchi kulipa ankara za maji kwa wakati ili kuwezesha mradi wa maji wa Same -Mwanha-Korogwe (SMK) kujiendesha kwa ufanisi na kuongeza mtandao wa huduma kwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SAMWASA, Mhandisi Rashid Mwinjuma amesema kuwa changamoto ya wizi wa maji inaisababishia mamlaka hiyo hasara kubwa kwa kuikosesha mapato, jambo linalokwamisha juhudi za upanuzi wa huduma kwa wananchi.

Ameeleza kuwaTaasisi hiyo itawachukulia hatua kali za kisheria watumishi wasio waadilifu wanaochangia hasara na kuharibu miundombinu ya maji, huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za siri pindi wanapobaini vitendo vya ubadhirifu au hujuma dhidi ya miundombinu ya maji.

Sheria ya kuunganisha maji bila kibali ni kosa la jinai linaloweza kusababisha mtu kushtakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhujumu Uchumi  na pia Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019.

Kwa mujibu wa sheria hizo, mtu yeyote anayejiunganishia maji kinyume cha taratibu, kuharibu miundombinu au kusababisha hasara kwa mamlaka ya maji, anatenda kosa linaloweza kumfikisha mahakamani na kuhukumiwa kwa kosa la jinai, ikiwa ni pamoja na kulipa faini au kifungo jela.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • DC KASILDA ATAKA WANANCHU KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI WAKATI WA ZIARA YA MWENGE WA UHURU

    June 10, 2025
  • WASHIRIKI UMISSETA WATAKIWA KUWAKILISHA VEMA WILAYA YA SAME

    June 09, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.