Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani Same Bw. Ninzari Idd ameshauri Wakulima kufuata kanuni Bora za Kilimo ili kuwawezesha kupata mavuno mengi na hivyo kuwa na Kilimo chenye tija.
Bw.Idd ametoa ushauri huo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya nanenane ambapo amesema mkulima akizingatia kuchagua mbegu bora, matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu ni lazima atapata mavuno mengi na yaliyo Bora.
Aidha amewataka Wakulima wanapopata changamoto za kilimo kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa ugani walio kwenye Kata na baadhi ya vijiji Wilayani humo.
"Tunao maafisa Ugani kwenye Kata zetu zote na baadhi ya vijiji hivyo ni vyema wakulima wakapata ushauri sahihi juu ya kilimo ili waweze kulima kilimo chanye manufaa"alisema Bw.Idd
Alisema wakulima wengi wamekuwa wakiendelea kulima kilimo cha mazoea ambacho huwapatia chakula cha familia tu jambo ambalo amesema sio sawa kwani mkulima anatakiwa alime kupata chakula na kupata mazao ya kuuza kwaajili ya kuongeza pato la familia.
Wilaya ya Same imeshiriki Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini 2025 kwenye viwanja vya Themi,Njiro Mkoani Arusha ambapo walipata fursa ya kuonesha na kutoa elimu juu ya mbinu mbalimbali za kuboresha kilimo na ufugaji.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.