NGO ya VOEWOF yadhamiria kuimarisha matumizi ya nishati mbadala Wilayani Same..
Katika kikao kilichofanyika Tar 20/03/2018. Wadau wa mazingira walieleza sababu zinazopelekea watu kutochangamkia nishati mbadala pamoja na juhudi za serikali na wadau kuhimiza matumizi yake.
kuendelea kuelimisha juu ya athari ya mazingira na uwepo wa nishati mbadala.
Shirika la VOEWOF linalofanya kazi chini ya CARE International linafanya kazi na vikundi vya wanawake.
limewezesha majiko ya gas zaidi ya 300 kutumika vijijini.
Limepania kuanzisha viwanda vya kutengeneza nishati mbadala kwa kutumia taka.
Wilaya yaahidi kutoa eneo, kutoa mikopo kwa vikundi hivyo na kutumia miti inayooteshwa na vikundi hivyo.
Kikao hicho pia kimewashirikisha DC wa Same, wataalamu toka ofisi ya RC Kilimanjaro na halmashauri ya Same, TBS, wanazuoni toka SUA, TRA, wauzaji wa nishati mbadala, wanavikundi hao na vyombo vya habari.
DC Same alipongeza na kuwashukuru VOEWOF Na wadau wengine jinsi wanavyoshiriki kuibadilisha Same, kila mmoja kwenye nyanja yake. Alikiri kuwa kwa kasi hii; Wilaya ya Same itafikia malengo yake ya kubadili mazingira ya Same.
" Same is not the same"
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.