Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusho Mapande wamekabidhiwa makombe sita ya ushindi wa UMISETA kimkoa ambapo mchezo wa mpira wa miguu(footbal) umeibuka kidedea na kushika nafasi ya kwanza.Mashindano hayo yalianza tarehe 7/6/2021 hadi leo tarehe 10/6/2021 katika shule ya Moshi technical.
Akipokea makombe hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Same Bi.Anastazia Tutuba amewapongeza sana wanafunzi hao na kuwaasa kuongeza juhudi katika michezo ili waibuke kidedea awamu ijayo.
Kulikuwepo pia na michezomingine kama kurusha kisahani michezo ya riadha na mingine mingi
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.