Katibu Tawala Msaidizi Utawala,Fedha na Ufuatiliaji Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Posencian Kirumbi ameipongeza Wilaya ya Same kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato.
Ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani ambapo alisema hata katika matumizi na usimamizi wa fedha za Serikali Wilaya ya Same imekua ikifanya vizuri na hivyo Kwa miaka mitano mfululizo imepata hati safi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Halmashauri ya Wilaya ya Same imeendelea kufanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 ikusanya Bil 2 sawa na asilimia 91.4 ya makisio , mwaka 2021/22 ilikusanya Bil 2.6 (101%) ,mwaka 2022/23 ilikusanya Bil 2.9 (109%) na mwaka Huu 2023/24 Halmashauri imelenga kukusanya Bil 3 ambapo hadi mwezi Machi 2024 imekusanya Bil 2.7
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.