Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Jimson Mhagama ametoa pongezi kwa Timu za Wilaya ya Same zilizoshiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2025 kwa kurejesha ushindi mnene.
Mkurugenzi alitoa pongezi hizo wakati akipokea vikombe vya ushindi toka kwa Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bw.Marclaud Mero akiwa pamoja Watumishi wa Idara hiyo.
Wilaya ya Same imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kwenye mashindano hayo na imejinyakulia Vikombe tisa vya ushindi.
Akitoa taarifa ya ushindi huo kwa Mkurugenzi, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Mwl.Marclaud Mero alisema Wilaya ya Same imeshika nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa Riadha , Goalball Wavulana na Sanaa za maonesho.
Aliitaja michezo mingine iliyoitoa Same kimasomaso kuwa ni pamoja na Basketball, Goalball Wasichana na Volleyball wasichana na wavulana ambazo zilishika nafasi ya pili kimkoa.
Mpira wa Miguu wasichana walishika nafasi ya tatu na Usafi Wilaya ilishika nafasi ya tatu.
Wilaya pia ilifanikiwa kutoa wanamichezo 31 ambao waliunda timu ya Mkoa na Kushiriki Mashindano hayo Ngazi ya Taifa.
Mkurugenzi ameipongeza Idara ya Elimu Msingi kwa kusimamia vema michezo.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.