Katika kufurahia ongezeko la takwimu za mabweni na madarasa katika chuo cha ufundi St.Joseph kinachomilikiwa na kanisa la RC jimbo la Same.
DC Same alieleza furaha yake ya kupata marafiki wazuri wanaojulikana kwa jina la Same.Ambao pia wana kiwanda cha matrekta kinachoitwa Same.Awashukuru kwa kushiriki dira ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati 2025 kwani Tanzania ya viwanda inataka mafundi mahiri.
Ampongeza Askofu Rogath Kimario kwa utashi wake mkubwa pamoja na kanisa katika kukuza elimu na kutangaza vizuri jina la Same na serikali yetu.
Naye Rais wa taasisi hiyo ya Foundazione Same,aeleza nia yake ya kuendelea kushiriki na kanisa RC Same katika kufikia malengo yao kadiri watakavyoshirikishwa.Hayo yote yalisemwa wakati wa uzinduzi wa vitu vilivyofadhiliwa na wadau hao toka Italy vikijumuishwa mabweni 2,madarasa 2,baiskeli 40 na trekta moja.
"Mchango huu mkubwa kwani leo tutabadilisha takwimu za mabweni na madarasa yaliyopo wilayani,sera nzuri za kushirikiana na wadau wenye nia njema na nchi yetu katika kuharakisha maendeleo"Alisema DC huyo.Ambapo pia aliwakaribisha wageni kuja kuwekeza wilayani Same na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.