• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

RC KILIMANJARO APONGEZA NA KUZINDUA MADARASA YA MPANGO WA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19 SAME DC

Posted on: December 18th, 2021

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Same amekabidhiwa na kuzindua vyumba 56 vya madarasa katika shule 36 za sekondari halmashauri ya Same, huku akiwapongeza wasimamizi wa mradi huo kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri, kata, viongozi wawakilishi wa wananchi pamoja na wananchi wote kwa ushiriki wao, kwa kukamilisha miradi hiyo kwa viwango na kwa wakati.

Mkuu huyo wa mkoa, ametoa pongezi hizo mara baada ya kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo alipokea na kuzindua madarasa 56, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua  miradi hiyo katika halmashauri ya Same.

"Ninawapongeza wananchi wote wa halmashauri ya Same kwa ushirikiano mliouonesha katika kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa madarasa, madarasa yamejengwa kwa viwango vinavyohitajika na kukamilika kwa wakati, madarasa yanavutia,  hii inaonesha dhahiri namna gani mnaunga mkono agenda ya mheshimiwa Rais, mama Samia ya kuboresha huduma za jamii na kuondoa kero kwa wananchi, hongereni sana ofisi ya mkuu wa wilaya, timu ya watalamu halmashauri, waheshimiwa madiwani pamoja na wananchi wote kwa ujumla wenu" amesisitiza Mhe. Mpogolo.

Aidha, mheshimiwa Mpogolo amewataka wananchi kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kuwa serikali imeleta fedha nyingi katika miradi ya elimu, afya, maji na barabara, serikali inahitaji ushiriki wa wananchi, ushiriki ambao utawezesha umiliki wa wananchi wa miradi hiyo baada ya kukamilika.

Katika ziara hiyo viongozi wawakilishi wa wananchi, wameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita na juhudu za mhesimiwa Rais, mama Samia Suluhu kwa kuelekeza fedha nyingi, kiasi cha shilingi bilioni 1,120 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za halamshauri ya Same, jambo ambalo wamekiri halijawahi kutokae na kuongeza kuwa, fedha hizo za ujenzi wa madarasa zimekuja wakati muafaka kwa kuwa kila mwaka, wananchi hulazimika kuchangishana kujenga madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka unaofuata.

Diwani wa kata ya Msindo Mhe. Yusto Mapande ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kuwa licha ya kuwa madarasa hayo yatawanufaisha watoto wao, lakini kwa kiasi kikubwa yamewapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishana fedha za ujenzi wa madarasa, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka nyakati kama hizo.

Ikumbukwe kuwa, halmashauri ya Same ilipokea shilingi bilioni 1,120 milioni, fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19,  za ujenzi wa vyumba 56 vya madarasa kwa shule za sekondari na madarasa yote yanatakiwa kukamilika ifikapo 31, Desemba, 2021.



SAME DC

Kazi Iendelee.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • MRADI WA SWASH ULIVYONUFAISHA WILAYA YA SAME

    April 03, 2025
  • WANANCHI WA MAKEI,SAME WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

    March 23, 2025
  • SAME YATOA ELIMU YA TAHADHARI YA MPOX MASHULENI

    March 18, 2025
  • MAAFISA UTUMISHI SIMAMIENI STAHIKI ZA WATUMISHI-DC SAME

    March 13, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.