Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa manunuzi ya Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini Bw.Magai Maregesi amekumbusha umuhimu wa kuhakikisha kuwa manunuzi yote ya Umma yanafanyika kupitia mfumo wa NesT.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Timu ya Menejimenti (CMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Same wakati wajumbe kutoka PPRA walipofanya ziara ya kikazi Wilayani Same.
"Wakuu wote wa Idara na Vitengo hakikisheni kuwa manunuzi yote yanafanyika kwenye mfumo wa NesT kuanzia kutangaza zabuni"alisema.
Hata hivyo baadhi ya wakuu wa Idara walilalamikia mfumo kuwa taratibu na wakati mwingine kutopatikana kwa siku nzima.
Bw.Maregesi alisema changamoto zilizokuwepo kwenye mfumo zimeshafanyiwa kazi na sasa mfumo wa NesT hauna changamoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama alipokea maelekezo hayo na kuahidi kutekeleza.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.