Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's)kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mkuu wa Wilaya ametoa wito huo wakati aliokua akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa mashirika hayo Wilayani Same.
“Pamoja na majuku yenu makubwa mnayotekeleza kwenye Wilaya ya Same lakini pia mna dhamana ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa" alisema Mhe.Kasilda.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wakazi wa Same kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu umebebwa na kaulimbiu isemayo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki”.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.