Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Bw.Jimson Mhagama leo amefika kujitambulisha Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni.
Mkurugenzi Mhagama amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,Singida kufuatia mabadiliko ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya yaliyofanywa Machi 09,2024 na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Bw.Mhagama pia aliweza kukutana na kufahamiana na wajumbe wa Timu ya Menejimenti Halmashauri (CMT) ya Wilaya ya Same.
Katika Uhamisho huo aliyekuwa Mkurugenzi wa Same,Bi.Anastazia Tutuba amehamishiwa Manyoni Mkoani Singida.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.