Mkuu wa wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stacki awataka wanawake kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu isemayo
"KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA; TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI"
Mhe.Rosemary Stacki amesema serikali ipo mstari wa mbele kumwezesha mwanamke katika elimu,ajira,siasa na uchumi.Vilevile awaasa wanawake wa same kuwalea watoto katika maadili mema ni jukumu lao ili kupunguza ndoa na mimba za utotoni.
Mwisho, Mhe.Rosemary Stacki asisitiza wadau washirikiane kuhakikisha vikundi vya wanawake vinaimarika.bofya hapa kuona maandamano
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.