Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg.Ismail Ali Ussi ameelezwa kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi nane ya ya Halmashauri ya Wilaya ya Same iliyofikiwa na Mwenge wa Uhuru iliyokuwa na thamani ya shilingi bilioni 2.7.
Akizungumza alipokuwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa maji Mroyo-Kizangaze, Maore Wilayani hapa Kiongozi huyo alisema utekelezaji wa Miradi yote iliyofikiwa na Mwenge imefanywa kwa kuzingatia taratibu zote muhimu za Serikali.
“Niwapongeze sana viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa usimamizi mzuri wa Miradi kwani tumekagua Miradi pamoja na nyaraka zake zote na hakuna mashaka yoyote tuliyokutana nayo,hongereni sana” alipongeza Ndg. Ussi.
Akizungumzia mbio za mwenge wa Uhuru Wilayani Same Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alisema ukiwa Wilayani Same Mwenge wa Uhuru ulizindua Kituo cha Mafuta cha Mayai (Tsh.mil.431) uliweka jiwe la Msingi Zahanati ya Masandare (Tsh.Mil 50.5) ambapo pia ulizindua barabara ya lami Same Mjini yenye urefu wa km 1.43(Tsh.mil.980.9)
Alisema Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Ismail Ali Ussi alipata nafasi ya kugawa majiko ya gesi 40 kwa wajasiriamali ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za matumizi ya nishati Safi ya kupikia,majiko hayo yalinunuliwa kwa shilingi milioni 1.9 ambazo zilitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mwenge wa Uhuru pia uliweka jiwe la Msingi kwenye Miradi wa Maji Mroyo-Kizangaze (Tsh.bil 1.1) na kuzindua Nyumba ya Mwalimu Shule ya Sekondari Misufini Goma (Tsh.mil 98.1)
Miradi mingine iliyofikiwa na Mwenge wa Uhuru Kikundi cha Wajasiriamali cha Vijana Welding chenye mtaji wa shilingi milioni 13.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru pia alipata fursa ya kugawa viti na meza 200 vyenye thamani ya shilingi milioni 22 kwaajili ya shule za Sekondari.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.