Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Same limepata Viongozi katika Mkutano wa Uchaguzi uliofanyika Septemba 11 kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Viongozi hao ambao watadumu madarakani kwa miaka mitatu ni Mwenyekiti Bi.Haika Nyange,Katibu Bi. Neema Daudi na Bi.Tatu Mkumbwa ambaye amechaguliwa kuwa Mweka Hazina.
Akizungumza kwenye Mkutano huo Afisa Mendeleo ya Jamii Wilaya ya Same Bw.Charles Anatoly aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi zao kuwatangazia wanawake fursa za kiuchumi zilizopo.
"Tujenge Jukwaa imara na tuwatangazie wanawake fursa za mitaji,mikopo,biashara na masoko ili wanawake waweze kujikwamua kiuchumi" alihimiza Afisa huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Wilaya ya Same Bi.Haika Nyange aliahidi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata taarifa zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.