Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Ndg.Tito Mganwa(TEA) na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Watumishi Housing Eng.Lwitiko Mwandobo(WHC) wameikabidhi nyumba ya kuishi walimu katika shule ya sekondari Vumari kata ya Vumari ambayo itatumiwa na familia sita(six in one),nyumba hiyo imegharimu Tshs.145,000,000/=
Akikabidhiwa nyumba hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Same Afisaelimu Sekondari Wilaya Bi.Happiness Laizer amewashukuru kwa mchango wao mkubwa wa kuwajengea waalimu nyumba za kuishi na familia zao amesema ni motisha kwa waalimu na itasaidia kwa wanafunzi wa Vumari sekondari kupata elimu bora zaidi.Sambamba na hayo Mkuu wa shule ya sekondari Vumari Bi.Odilia Mushi ametoa shukrani kwa uongozi na mamlaka ya elimu Tanzania kwa kuwajengea walimu nyumba za kuishi.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.