• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

DKT MPANGO AITAKA WIZARA YA MALIASILI KUFANYA TAFITI KUPATA NJIA MBADALA WA MKAA NA KUNI

Posted on: March 22nd, 2024


Makamu wa Rais, Mhe.Dk. Philip Isdor Mpango ameitaka  Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi zake  na wadau wa Mazingira kufanya tafiti za namna ya kupata  teknolojia za kisasa zitakazopunguza matumizi ya mkaa na kuni kama nishati ya kupikia ili kunusuru uharibifu wa Misitu.

Akizungumza Wilayani Same,Kilimanjaro Machi 21,2024 katika  Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Upandaji wa Miti Kitaifa, Dkt. Mpango amesema sekta ya Misitu nchini Tanzania bado inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo uharibifu mkubwa wa maeneo ya Hifadhi, hali inayochochea mabadiliko ya tabia nchi.

 Amesema matumizi ya nishati chafu (kuni na mkaa) hapa nchini yameendelea kuwa kichocheo kikubwa cha ukataji holela wa miti na uharibifu wa Hifadhi za misitu, changamoto ambayo inabidi kukabiliwa haraka iwezekanavyo.

“Takwimu zinaonyesha kuwa, katika kila kaya 10 nchini Tanzania, kaya 9 zinatumia nishati ya kuni na mkaa, hii ni changamoto kubwa ambayo lazima wizara husika ishirikiane na Taasisi zake na wadau katika kuikabili,” alisema.                                  

Ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAMISEMI, Chuo cha Olmotonyi , Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kushirikiana kwa dhati na wadau wengine  katika kubuni teknolijia ya kisasa itakayosaidia katika kudhibiti uharibifu wa rasilimali za misitu nchini Tanzania.

“Tafiti na teknolojia hizo ni lazima zilenge katika jitihada za kuvumbua nishati mbadala nyepesi na rafiki, lakini pia, tunahitaji kuwa na teknolojia rafiki itakayosaidia zao la tumbaku kukaushwa bila uharibifu wa mazingira,” Dkt. Mpango aliagiza.

Makamu wa Rais amezitaka Wilaya na Halmashauri zote nchini kutenga maeneo mengi ili kuruhusu miti kupandwa kwa wingi zaidi, huku akiwaelekeza Wakurugenzi wa Majiji ,Miji na Halmashauri hapa nchini kuanzisha bustani nzuri za miti kwa ajili ya mapunziko na mazoezi.

Awali akimkaribisha  mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alisema kuwa Sekta  ya Misitu inachangia asilimia 3.5 ya pato la Taifa, ikiwa pamoja na asilimia 10 ya ajira kwa Watanzania.

Waziri Kairuki alisema dhumuni la Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa, pamoja na mambo mengine ni kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa upandaji na utunzaji miti, na kuongeza, kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ya ‘Misitu na Ubunifu’ kauli inaonyesha dhamira njema ya Serikali katika kukuza sekta ya misitu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amesema Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa ni siku muhimu sana kwa Taifa na wakazi wa Kilimanjaro, na Wilaya ya Same na Taifa zima kwa ujumla.

Amesema mpaka sasa Mkoa wa Kilimanjaro umefanikiwa kupanda zaidi ya miti milioni 8, na kwamba wameweka mikakati mbalimbali endelevu ya kuhakikisha miti hiyo inatunzwa vyema kwa  kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi ya wafugaji wenye tabia ya kulisha mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • WANANCHI WAONYWA KUTOJIUNGANISHIA MAJI KWA NJIA ZISIZO RASMI

    June 18, 2025
  • DC KASILDA ATAKA WANANCHU KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI WAKATI WA ZIARA YA MWENGE WA UHURU

    June 10, 2025
  • WASHIRIKI UMISSETA WATAKIWA KUWAKILISHA VEMA WILAYA YA SAME

    June 09, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.