Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bw.Jimson Mhagama ameushukuru Ubalozi wa Japan hapa nchini kwa kutoa Milioni 281.3 kufadhili Ujenzi wa Zahanati ya Malindi iliyopo Kata ya Siku Wilayani hapa.
Mkurugenzi Mhagama ametoa shukrani hizo wakati mwakilishi wa Balozi wa Japan Bi.Chika alipofika kutembelea Zahanati ya Malindi.
Ujenzi wa Zahanati ya Malindi umegharimu Jumla ya Shilingi Milioni 470.26 ambapo imejumuisha Ufadhili huo wa Japan kupitia Miradi wa Msaada wa kuwezesha Usalama wa wananchi wa Vijijini (Grant Assistance for Grassroots Human Security Project).
Ufadhili mwingine wa Shilingi Milioni 38.6 umetolewa wa Serikali Kuu kupitia Miradi wa maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSSP)
Halmashauri ya Wilaya ya Same kupitia fedha za mapato ya ndani ilichangia Shilingi Milioni 37.3 ambapo nguvu za wananchi ni Milioni 113.
Katika awamu ya kwanza ya ujenzi ufadhili huu umefanikisha Ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje ambalo linajumuisha wadi ya mama,Baba na mtoto,huduma za uzazi,Ujenzi wa Choo cha matundu manne pamoja na ununuzi wa samani pamoja na Ujenzi wa Nyumba moja ya Mtumishi.
Awamu ya pili ambayo itakamilika Agosti mwaka imejumuisha Ujenzi wa kichomea taka,shimo la kutupa kondo la nyuma,shimo la majibu na sehemu ya kunawa mikono.
Zahanati ya Malindi imesajiliwa na imeshaanza kutoa huduma na tayari imeshahudumia wananchi zaidi ya 650O.
Kwa upande wake Bi.Chika aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa kusimamia vema utekelezaji wa Mradi huo ambao umeondoa changamoto ya wananchi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za matibabu.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.