• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

DC KASILDA AWAASA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUZINGATIA MAADILI

Posted on: September 30th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchanguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Jimbo,Kata na Vijiji kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma wakati wote watakapokuwa wanasimamia Uchaguzi huo.

Mheshimiwa Kasilda ametoa angalizo hilo wakati akifungua mafunzo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wasidizi ngazi ya Kata na Vijiji ambapo alisema njia pekee ya kufanya kazi hiyo kwa uadilifu ni kwa kuzingatia miiko ya utumishi wa umma.

“Ukizingatia maadili ya utumishi wa Umma  utaepuka rushwa,utafanya kazi kwa weledi na kujituma,utaweza kutunza siri za ofisi na utakuwa Mzalendo kwa Taifa lako” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha amewahimiza Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zote sahihi kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kushiriki kikamilifu katika hatua zote zinazowahusu ikiwemo kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura.

“Hakikisheni mnasoma miongozo yote ya uchaguzi na kuielewa ili muweze kutekeleza jukumu hili kwa weledi na pia zingatieni ratiba iliyotolewa ya Uchaguzi na muifuate ili msiwe mbele wala nyuma ya ratiba” alisema.

Akizungumza katika mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi Bw.Jimson Mhagama amewataka wasimamizi wasaidizi hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi 134  ngazi ya Kata na Vijiji yalitanguliwa na kula kiapo cha uadilifu ambapo Hakimu Levina Masha aliwaapisha.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Hapa nchini unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo Oktoba 11 hadi 20 kutakuwa na zoezi la wapiga kura kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • MRADI WA SWASH ULIVYONUFAISHA WILAYA YA SAME

    April 03, 2025
  • WANANCHI WA MAKEI,SAME WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

    March 23, 2025
  • SAME YATOA ELIMU YA TAHADHARI YA MPOX MASHULENI

    March 18, 2025
  • MAAFISA UTUMISHI SIMAMIENI STAHIKI ZA WATUMISHI-DC SAME

    March 13, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.