Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Same wameibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu hapa nchini.
Akitoa taarifa ya matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Same Bw. Charles Anatoly amesema CCM imeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi huo.
Bw.Anatoly amesema zoezi zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Wilaya ya Same limeenda vizuri ambapo hali ya usalama ilikuwa nzuri na Zaidi ya asilimi 95 ya wananchi waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura.
Bw.Wiljon Kibiriti ni mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji kwenye kijiji cha Msindo ambaye alipeperusha vema bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye anasema kuwa kazi ya kufanya kampeni haikuwa ngumu kwani utekelezaji wa Miradi umefanyika kwa kiasi kikubwa hivyo kuendelea kuimarisha Imani ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nikiwa mkweli utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo umesaidia kwa kiasi kikubwa kutupa ushindi sisi wagombea wa CCM, wananchi walio wengi wana Imani na Chama Cha Mapinduzi” alisema Mwenyekiti huyo.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti 100 vya nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji, nafasi 503 za wenyeviti wa vitongoji na wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.