Monday 23rd, May 2022
@Kasapo-Makanya
Tukio la tembo kuua mwananchi mmoja na ng'ombe ambapo kitengo cha wanyamapori kilikuwa kwenye zoezi la kudhibiti mnyamapori hatari aina ya tembo mmoja dume aliyekuwa katika makazi ya watu katika kata ya makanya.Juhudi za kumdhibiti zilifanyika kwa kumfukuza kurudi kwenye hifadhi.Kwa bahati mbaya tembo huyo alileta madhara tarehe 08/10/2018 kwa kuua ng'ombe mmoja majira ya saa 9 alfajiri katika kitongoji cha Nkwini,kijiji cha Makanya.Katika kumdhibiti asilete madhara zaidi tembo huyo dume alifukuzwa hadi kijiji cha Kasapo uelekeo wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi,kwa bahati mbaya alikutana na mwananchi ambaye alikuwa akitoka shambani na kumshambulia hadi kupelekea umauti wake.Mwananchi alijulikana kwa majina ya Athumani Habibu Msambaa mwenye umri wa miaka 35 na aliyekuwa akijishughulisha na kilimo.
Hali kadhalika wananchi na viongozi walitahadharishwa juu ya kuchukua tahadhari za kujilinda na kutoa taarifa haraka kwa kitengo husika endapo mnyamapori atakapoonekana kwenye maeneo yao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.