Thursday 28th, March 2024
@ruvu
"Nitakuwa mwaminifu kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Nitakuwa Mtii kwa Amiri Jeshi Mkuu pamoja Na Majeshi yote".
Hayo ni baadhi ya Maneno yaliyotamkwa Na vijana 160 wa Kata ya Ruvu Wilaya ya Same, kama sehemu ya kiapo cha utii wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba Tar. 05/01/2018.Vijana hao walioshiriki mafunzo kwa muda wa miezi 5, walionekana kuwa jasiri, wakakamavu, Na ari kubwa ya kuitumikia nchi yao.Naye Mkuu wa Wilaya ya Same aliyekuwa mgeni rasmi alieleza yafuatayo:
1. Furaha ya Taifa, Mkoa na Wilaya kuongeza watu wazalendo Na waliotayari kuitete nchi yao kwa gharama yoyote.
2. Kata ya Ruvu ni kati ya kata zilizokuwa Na migogoro ya wakulima & wafugaji. Ni matarajio yetu kupitia vijana Hawa 160 migogoro itakwisha.
3. Vijana Hawa waunde vikundi vya uchumi kama ujenzi, Kilimo Nk. Idara ya M/jamii ifanye kazi.. Ili baadaye wapewe mikopo.
4. Kila Kijiji kiliagizwa kutenga heka 100 kwa ajili ya vijana. Wapewe Hawa eneo.
5. Viongozi wa vijiji, kata Na polisi kuwatumia vizuri
6. Wahitimu kuzingatia kiapo chao kwa vitendo, swala la kujitolea Na mengine.
7. Serikali Tutaendelea kuwapa kipaumbele kunapotokea uhitaji Na kampuni za ulinzi kuajiri waliopitia mafunzo haya.
8. DC alitoa Tshs. 50,000/= kwa kila mshindi kwa washindi 10.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.